Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: kiongozi huyo amekwenda nchini humo akifuatana na viongozi wenzake kwaajili ya kutoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa wa tukio la siku ya Qudsi pia ikiwemo kuonana na kiongozi wa mashia wa nchi hiyo Sheikh Zakizaki ambaye amepoteza watoto watatu katika tukio hilo ambalo kwaujumla limesababiksha vifo vya watu 33 nchini humo.
Viongozi hao ni Hujatul Islamu walmuslimina Akhtariy (katibu mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya Ahl al-Bayt(a.s)), Mh Muhammad Shakiba (kutoka katika ofisi ya kiongozi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran) Dr Muhammad Hasan Tabaraiyan (kiongozi msaidizi wa jumuiya ya kimataifa ya kukurubisha Madhehebu ya kiisalimu) na Mh Hasan Khakrand (msimamizi wa masuala ya Afrika katika jumuiya ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) na msafara huo uliwasili nchini Nigeria wiki iliopita.
Viongozi hao Baada ya kuwasili mjini Lagos walipitia mkoani Kanu nahatimae kuingia wilayani Zariya ambapo ndiko kulikotokea mauaji ya siku ya Qudsi nakupokewa msafara huo na kiongozi wa harakati za Kiislamu nchini Nigeria Sheikh Zakizaki.
msafara huo baada ya kufika nchini Niegeria uliongozana na balozi wa Iran nchini Niegeria (Mh Saidi Kuzih Chiy) nakuwasili nyumbani kwa Sheikh Zakizaki nakutoa salamu za rambirambi kwa familia yake kwa kufiwa na watoto zake watatu wakiume katika mauaji hayo yaliofanyika siku ya Qudsi
Akhtariy baada ya hapo alihudhuria katika Husainiyah ya Baqiyatullah wilayani Zariya kwaajili ya kuonana na waumini waliopoteza watoto zao katika mauwaji ya siku ya Qudsi naye baada ya kusali sala ya jamaa alipewa nafasi yakuzungumza na waumini waliohudhuria naye akazungumzia tukio la mauaji yakinyama yaliotokea nchini humo nakutoa rambirambi kwafiwa kisha kuelezea nafasi ya mashahidi mpele ya mwenyezi Mungu mtukufu.
Baadaye sheikh Zakizaki alitoa shukurani zake za dhati kwa katibu mkuu wa jumuiya ya kimataifa ya AhlulBayt (a.s) na wenzake aliofuatana nao, aidha alitoa shukurani kwa maulamaa, Taasisi na shahsiya zote ziliotoa rambirambi nakushiriki pamoja nasi katika majonzi yaliotkuta katika siku ya kimataifa ya Qudsi.
Katibu mkuu huyo baada ya kubaki wilyani Zariaya siku moja pamoja na wenzake walisindikizwa na Sheikh Zakizaki nakurudi nchini Iran siku ya ijumaa sambamba na tarehe 8 agosti.